soundcloud

SAHAMA HAMAD 18 - Pata taarifa mbalimbali za Kisiasa, Uchumi, Dini pamoja na simulizi mbali mbali za kusikitisha zikiambatana na Makala pamoja na Tahrir za Kusisimua.. Pia tuwasiliane kupitia +255659887692 AHSANTENI...

Thursday, 9 April 2015

AJALI MBAYA YATOKEA JANA MJINI TANGA

 
 ajali iliyohusisha magari matatu likiwemo la Ratco hapo jana na kupelekea watu kumi kufariki dunia likihusisha Basi la Ngorika lenye namba za Usajili T770 BKW lililokuwa kitoka jijini Dar es Salaam kwenda Arusha na lile RATCO lililokuwa likitokeaTanga kwenda Dar es Salaam yakigongana uso kwa huso na kulihusisha gari lingine dogo aina ya Toyota Pass T 628 CXE na kusababisha vifo vya abiria 10 na majeruhi zaidi ya 35,ajali hiyo ikitokea eneo la Mbweni Mkata, wilayani Handeni mkoni Tanga huku chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo iliyokuwa likitaka kulipita lori lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.

Taarifa zinaeleza zaidi waliofariki katika ajali hiyo ni kutoka katika gari la Ngorika watu 7 na lile Dogo watu 3 lakini katika Gari la Ratco abiria wamepata majeruhi na wanaendelea kupata matibabu huku wengine wakiruhusiwa...