Mcheza
tenis wa Uingereza Andy Murray amefanikiwa kuingia nusu fainali baada
ya kumshinda Dominic Thiem raia wa Austria katika mashindano ya Miami
Open yanayoendelea huko nchini Marekani.
Pamoja na kupoteza seti ya kwanza ya mchezo huo,Murray alifanikiwa kuzinduka na kushinda kwa jumla ya seti 3-6 6-4 na 6-1.Murray mwenye umri wa miaka 27, anaweza kupambana na Tomas Berdych raia wa Czech ama Muajentina Juan Monaco katika nusu fainali ya mashindano hayo.
