soundcloud

SAHAMA HAMAD 18 - Pata taarifa mbalimbali za Kisiasa, Uchumi, Dini pamoja na simulizi mbali mbali za kusikitisha zikiambatana na Makala pamoja na Tahrir za Kusisimua.. Pia tuwasiliane kupitia +255659887692 AHSANTENI...

Monday, 20 April 2015

Vijana nchini Watakiwa kujiunga katika vikundi ili kujikomboa Kiuchumi


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone  katikati akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo ulipotembelea Mkoa huo kwa lengo la kutoa elimu kwa  vijana ya jinsi ya kujikomboa kiuchumi .Wa kwanza kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Uhamasishaji na Uwezeshaji Kiuchumi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dr. Steven Kissui .
Maafisa Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Idara ya Maendeleo ya Vijana waliosimama wakifundisha jinsi ya kuandika mchanganuo wa Mradi.Mafunzo hayo yalifanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Mkoa wa Singida hivi karibuni

Imeelezwa kuwa jukumu kubwa la Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ni kuratibu mapambano dhidi ya biashara , matumizi , uingizwaji na usafirishaji wa dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kutoa taaluma kwa jamii pamoja na kutoa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watumiaji wa dawa za kulevya .

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dr Omar Dadi Shajak wakati akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa robo ya tatu  kuanzia Januari hadi Machi kwa kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa Serikali  kwenye ukumbi wa mikutano  Ofisini Makamu wa Kwanza wa Rais migombani .

Dr  Shajak amesema katika kupunguza  uingizwaji na usafirishaji wa dawa za kulevya Tume imetowa mafunzo ya sheria ya dawa za kulevya kwa taasisi mbali mbali zilizomo kwenye mapambano hayo kama vile Polisi , waendesha mashtaka , mahakimu , watumishi wa viwanja wa ndege , bandari, TRA, ZRB.

Lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa wa sheria ya dawa za kulevya na kuimarisha mashirikiano kisekta katika mapambano ya Dawa za Kulevya aidha kwa upande wa taaluma kuhusu athari ya Dawa za Kulevya imetolewa kwenye Shehia na baadhi ya Skuli na sehemu za kazi .

No comments:

Post a Comment