Meza kuu katika maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa
Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji,
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Bw. Ernest
Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika
mkoani Morogoro.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Meza
kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka
kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari
nchini (UTPC), Jane Mihanji, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari
Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),
Alvaro Rodriguez.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza
katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimio hayo.]
Kaimu
Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo
vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani.
Kutoka
kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na
Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu
wakifuatilia mijadala katika mkutano huo.
Mwanahabari na Bloga, Maggid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza.
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.[/caption]

UMOJA wa Nchi za Ulaya nchini
Tanzania (EU) umepinga vikali vitendo vya kikatili na unyanyasaji
ambavyo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari na vyombo vya dola vya
Serikali wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ambapo ilitokea
mwanahabari mmoja kuuwawa. Alisema hawatachoka kukemea matukio hayo ya
unyanyasaji kwani yanafifisha uhuru wa habari.
Akizungumza jana mjini Morogoro
katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kiongozi Mkuu
wa Mabalozi hao, Balozi Filiberto Sebregondi alisema EU itaendelea
kupinga namna yoyote ya unyanyasaji kwa wanahabari makundi yote wakiwemo
wa mitandao ya kijamii hadi utakapo kuwepo uhuru kamili wa vyombo vya
habari.
"...Tulifanya hivyo kwa mauaji
yalipotokea na tutaendelea kufanya hivyo siku zote watakapo kamatwa na
kupigwa wakiwa kazini...Tunajua huenda haitoshi lakini hii ni kutokana
na tofauti mbalimbali za kiutendaji," alisema Balozi Sebregondi.
Alisema kupinga unyanyasaji kwa
wanahabari haina maana wanachoandika wanahabari mara zote ni cha kweli
lakini ipo namna nzuri ya kushughulikia mvutano kama huo na kusaidia
kupata taarifa za kina zaidi zitakazofikia muafaka.
Aidha kwa upande wake Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ambaye alikuwa
mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alisema Tanzania inaongoza Afrika kwa
kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa udhibiti mawasiliano.
Alisema vyombo vya habari ni muhimu
katika taifa na hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Taifa unaotarajia
kufanyika Oktoba, alisema vyombo vya habari vinaweza kubomoa au kujenga
taifa lolote. "...Waandishi ni watu muhimu katika kudumisha demokrasia
nchini hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kujifunza zaidi.
Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya
habari duniani kitaifa yamefanyika mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na
wanahabari mbalimbali, wakongwe, wadau anuai wa vyombo vya habari huku
yakiwa na kauli mbiu ya Usalama wa Vyombo vya Habari katika Dijitali:
Uhandishi Mzuri unaozingatia, Usawa wa Kijinsia na faragha.