soundcloud

SAHAMA HAMAD 18 - Pata taarifa mbalimbali za Kisiasa, Uchumi, Dini pamoja na simulizi mbali mbali za kusikitisha zikiambatana na Makala pamoja na Tahrir za Kusisimua.. Pia tuwasiliane kupitia +255659887692 AHSANTENI...

Monday, 30 November 2015

Shekh ponda nje

BREAKING NEWS: Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia

Makosa yaliyokuwa yakimkabili ni mawili ambayo ni kushawishi watu kutenda kosa, pamoja na kutoa matamshi yanayoumiza imani ya dini nyingine.

Hakimu wa kesi hiyo Mary Moyo amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukujitosheleza hivyo mahakama hiyo imemwachia huru na rufaa iko wazi endapo upande wa mashitaka hautaridhika na hukumu hiyo.

No comments:

Post a Comment