#ZANZIBAR YA MWAKA 2010 IPO WAPI?
Visiwa vya Zanzibar ni visiwa ambavyo Allah amevijalia neema nyingi ambazo hupatikana katika visiwa hiyo mimea ya kila aina yenye kustawi ardhi, ubluu wa bahari yenye kila aina ya neema, jamii ya Watu walio na ustaarabu na busara na vingi vyenginevyo pamoja na kujalia zao kubwa la kibiashara la karafuu lenye kuingiza pato kubwa la mapato, vivutio vya kila aina ambavyo huwafanya watali kujaa katika visiwa hivyo kila mwaka.
Vitu hivyo vyote pamoja na vyengine vingi huaribiwa na chuki za kisiasa, zinazosababisha na baadhi ya Watu wenye kujali maslahi ya matumbo yao na kuwacha ukaribmu, busara walizokuwa nazo Watu wa visiwa hivyo vya Unguja na Pemba.
Tunafahamu ya kuwa siasa za uhasama zilianza kipindi kirefu visiwani humo tokea pale mfumo wa vyama vingi ulipoanza na kuendelea kwa miaka kadhaa.
Lakini ahuweni tuliipata pale viongozi wazalendo wa taifa hilo walipotoa tofauti zao za kisiasa na kuangalia Zanzibar yao kwanza na kufanikiwa kuondoa chuki na uhasama walizokuwa nazo wananchi wa visiwa hivyo.
Ukweli usiofichika Dr amani abeid amani karume aliyekuwa rais wa Zanzibar kati ya mwaka (2000-2010) na katibu mkuu wa Cuf maalim seif Sharif hamad walionesha uzalendo wao kwa kuwaleta wananchi wa visiwa hivyo kuwa wamoja na kufanikiwa kuwaondoa katika misingi ya chuki,uhasama, na ubaguzi wa uunguja na upemba waliokuwa nao wakazi wa visiwa hivyo.
Viongozi hao walifanya kazi kubwa ya kuwaunganisha wazanzibar na kuhakikisha wanawafanya wazanzibar waweze kupendana na kuthaminiana na kujiona kwamba wao ni wamoja.
Ukweli ulidhihirika katika uchaguzi uliofuta wa mwaka 2010 kuanzia kwenye kampeni za uchaguzi huu mpaka pale matokeo ya urais yalipotangazwa ambapo tuliona upendo waliokuwa nao wazanzibar kwa kuondoa uccm na ucuf waliokuwa nao na kuweka uzanzibar kwanza.
#INAENDELEA
No comments:
Post a Comment