Gazeti la "Süddeutsche" limeandika juu ya mashambulio yaliyofanywa na magaidi kwenye nyumba ya makumbusho katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis.
Gazeti hilo linatufahamisha juu ya umuhimu wa nyumba hiyo ya Makumbusho inayoitwa Bardo . Makumbusho hayo yanaonesha historia ya Warumi waliokuwa tajiri wakubwa katika karne za 2 na nne, wakati ambapo Yesu Kristo alikuwa bado hajazaliwa.
Gazeti la "Süddeutsche" linafahamisha zaidi nkwamba Makumbusho ya Bardo ya mjini Tunis yanakumbusha enzi za Punik,wakati wa vita vya mara kwa mara kati ya Roma na Kathargo yaani
Tunisia ya zamani.Gazeti la "Südeutsche" linaiita nyumba ya makumbusho ya Bardo ,hazina ya Afrika.
