soundcloud

SAHAMA HAMAD 18 - Pata taarifa mbalimbali za Kisiasa, Uchumi, Dini pamoja na simulizi mbali mbali za kusikitisha zikiambatana na Makala pamoja na Tahrir za Kusisimua.. Pia tuwasiliane kupitia +255659887692 AHSANTENI...

Saturday, 25 April 2015

HISTORIA YA SIKU YA LEO JUMAA MOSI 25 4 2015

Leo ni Jumamosi tarehe 6 Rajab mwaka 1436 Hijria inayolingana na tarehe 25 Aprili mwaka 2015 Miladia.
Jumamosi, Aprili 25, 2015
Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 5 Ordibehesht mwaka 1359 Hijiria Shamsia, Marekani ilishambulia kijeshi ardhi ya Iran kwa kutumia helikopta na ndege kadhaa za kivita. Serikali ya Marekani ilifanya mashambulizi hayo baada ya kushindwa njama zake mbalimbali za kutaka kuuangusha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran. Lengo la mashambulio hayo lilikuwa ni kutaka kuwakomboa majasusi wake waliotiwa mbaroni wakati wa kutekwa ubalozi wa Marekani hapa nchini uliokuwa pango la kijasusi. Licha ya kuweko mipango makini, kutumiwa vyombo vya kisasa kabisa na mazoezi mengi yaliyofanywa katika eneo linalofanana na hilo ili kuhakikisha operesheni hiyo inafanikiwa, lakini mashambulizi hayo yalikatishwa na tufani kubwa ya mchanga iliyotokea Tabas na kupelekea kuanguka baadhi ya ndege, kushika moto helikopta za Marekani na kufa baadhi ya askari wa nchi hiyo huku waliobakia wakiikimbia ardhi ya Iran. ***

Miaka 44 iliyopita katika siku kama ya leo, Wamarekani laki mbili walifanya maandamano mjini Washington wakiendeleza upinzani wao dhidi ya mashambulizi ya nchi hiyo huko Vietnam. Maandamano hayo yalikuwa miongoni mwa vielelezo vikubwa vya upinzani wa wananchi wa Marekani dhidi ya siasa za kichokozi za serikali ya nchi hiyo huko Vietnam. Katika vita vya Vietnam vilivyoanza mwaka 1964 Marekani ilituma askari laki tano nchini humo ambako maelfu miongoni mwao waliuawa na kujeruhiwa. Kwa sababu hiyo wananchi wa Marekani walizidisha upinzani dhidi ya vita hivyo na mwaka 1975 Marekani ililazimika kufunga virago na kuondoka Vietnam kutokana na mashinikizo ya ndani na ya kimataifa na kushindwa mara kwa mara jeshi la nchi hiyo katika medani za vita. ***

Katika siku kama ya leo 920 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, alifariki dunia Abu Muhammad Qassim bin Basri maarufu kwa jina la Ibn Hariri, mwanafasihi na mwandishi wa Kiirani aliyekuwa akiishi Basra. Ibn Hariri ndiye aliyeandika kitabu cha Maqamaat, kitabu ambacho ni cha aina yake. Katika kitabu hicho amebainisha kwa lugha nyepesi visa na hekaya zilizojaa mafundisho