
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa Habari
leo jijini Dar es salaam. Maadhimisho ya mwaka huu yatapambwa na Kauli
Mbiu isemayo Miaka 51 ya Muungano, Tudumishe Amani Na Umoja ,Ipigie Kura
ya Ndiyo Katiba inayopendekezwa na Kushiriki Uchaguzi Mkuu.
Askari
wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Maji wakipita mbele ya jukwaa kuu la
uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo jijini Dar
es salaam.
Askari
wa Kikosi Maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Komando) wakipita
mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.
Na. mwandishi wetu
Serikali
imesema kuwa maandalizi ya Sherehe za Miaka 51 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar yamekamilika na kwamba sherehe hizo
zitafanyika katika uwanja wa Uhuru Aprili 26 mwaka huu.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya sherehe hizo kwa niaba
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam leo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia
Mjema amesema maadhimisho ya mwaka huu yatapambwa na Kauli Mbiu isemayo
Miaka 51 ya Muungano, Tudumishe Amani Na Umoja ,Ipigie Kura ya Ndiyo
Katiba inayopendekezwa na Kushiriki Uchaguzi Mkuu.
Amesema
Tanzania katika kipindi cha miaka 51 ya Muungano imepata mafanikio
makubwa katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ya jamii, uchumi,
Siasa,Ulinzi, Usalama na Uhusiano wa Kimataifa


