Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na upepo mkali huko Kisiwa Panza, Wilaya ya Mkoani Pemba (Picha na mwandishi wetu)
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
amewapongeza wananchi wa Kisiwa Panza kwa mshikamano waliouonesha wakati
yalipotekea maafa ya upepo mkali Jumatano iliyopita.
Amesema
mshikamano huo unadhihirisha jinsi wananchi wanavyoweza kushirikiana
katika masuala ya kijamii na kuweka kando tofauti za kisiasa ambazo mara
nyingi huwagawa wananchi.
Maalim
Seif ameeleza hayo baada ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na upepo
huo, na kuelezea kufarajika kwake kwa jinsi wananchi walivyoweza
kushirikiana katika kukabiliana na maafa hayo.
Amesema
umoja na mshikamano ndio msingi imara wa kuleta maendeleo katika jamii,
na kuwataka wananchi kuendeleza utamaduni huo wa mashirikiano wakati
wowote yanapotokea masuala ya kijamii.
Akizungumza
katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdallah,
amesema jumla ya nyumba ishirini na tano (25) na familia mia moja na
kumi na nne (114) zimeathirika kutokana na upepo huo uliovuma usiku wa
kuamkia tarehe 22/04/2015.
Amesema athari nyengine zimetokea kwa vipando vikiwemo migomba pamoja na miti mbali mbali ikiwemo miembe na mikarafuu.
Mapema
akitoa neno la shurani kwa niaba ya wananchi waliokumbwa na maafa hayo
Bw. Faki Makame Faki ameishukuru seriakali kwa kuwaunga mkono katika
maafa hayo.
Ameiomba
serikali kuendelea na moyo huo kwa wananchi wakati wote yanapotokea
maafa, na kuahidi kuwa misaada inayotolewa itatumika kuwasaidia wananchi
walioathiriwa na upepo huo.
Maalim
Seif ameungana na wadau wengine kusaidia gharama zilizotokana na maafa
hayo na ameahidi kuchagia shilingi milioni tatu (3,000,000).


