soundcloud

SAHAMA HAMAD 18 - Pata taarifa mbalimbali za Kisiasa, Uchumi, Dini pamoja na simulizi mbali mbali za kusikitisha zikiambatana na Makala pamoja na Tahrir za Kusisimua.. Pia tuwasiliane kupitia +255659887692 AHSANTENI...

Saturday, 4 April 2015

MAN U YASHINDA, ARSENAL KICHEKO

Arsenal yaibana Liverpool,Man U yashinda
   manchester United
Arsenal imeimarisha uongozi wao wa kushiriki katika mechi za vilabu bingwa barani Ulaya baada ya kuicharaza Liverpool mabao 4-1 katika uwanja wa Emirates.

The Gunners iliweka wazi lengo lao la kuchukua pointi zote tatu baada ya kufunga mabao matatu ya haraka katika dakika nane za mwisho za kipindi cha kwanza kupitia Hector Bellerin,Mesut Ozil,na Alexi Sanchez huku mshambuliaji Olivier Giroud akipiga msumari wa mwisho wa jeneza la Liverpool alipofunga bao la nne katika kipindi cha pili.
Arsenal
Wakati huohuo Manchester United imeishinda Aston Villa mabao 3-1 na kupanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza. Kipa wa Aston Villa Brad Guzan alipangua mkwaju uliopigwa na mlinzi Marcos Rojo lakini
alifungwa na Anders Herrera baada ya kazi nzuri kutoka kwa Daley Blin

Wayne Rooney aliongeza bao la pili alipofunga katika kona ya mlingoti wa goli. Hatahivyo Villa walipata bao la kufutia machozi kupitia mshambuliaji wao Benteke huku Anders Herrera akifunga udhia.