Jaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.
Dk. Benson Bana wa
Chuo Kikuu cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa
amewataka wadau wa siasa na wananchi kwa ujumla kuzuia uvunjifu wa amani
kuelekea uchaguzi mkuu kwa kufuata Sheria na kutobeza mamlaka.
Dk Bana alisema
hayo jana akijibu swali la msimamizi wa mdahalo wenye lengo la
kuimarisha demokrasia ya vyama vingi ulioandaliwa na Msajili wa Vyama
vya siasa kwa ufadhili wa UNDP, Profesa Bernadetta Killian.
Profesa Killian
alitaka kujua baada ya maelezo ya awali ya Dk Bana juu ya mtazamo wake
kuhusu ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania , nini
kinastahili kufanya kuepuka uvunjifu wa amani hasa katika muda huu
ambapo viashiria vipo.
Dk Bana alisema
kama watu hawatafuata utamaduni wa vyama vingi, utamaduni wa kufuata
sheria na kutobeza mamlaka, taifa litaingia katika machafuko.
Alisema watu kama
wanaona wanaonewa wanatakiwa kufuata taratibu na kama taratibu hizo
zinaonekana ni tatizo bado wanatakiwa kuwa na subira na kuondoa taratibu
hizo zenye matatizo kwa kufuata utaratibu.
Katika shauri hilo
la viashiria vya mizozo Profesa Rugumamu, aliyebobea katika masuala ya
kutanzua mizozo aliihimiza Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa
kutengeneza mfumo wa utambuzi wa viashiria vya hatari (early warning)
ili iweze kukabiliana navyo mapema.