Mwenyekiti
wa CUF zoni ya Mjini Unguja Massoud Khamis, akimkabidhi fedha taslim
Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, ili aweze kuchukua
fomu ya kugombea urais wa Zanzibar wakati utakapofika.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akionyesha fedha alizokabidhiwa kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais.
Mwenyekiti
wa CUF zoni ya Mjini Unguja Massoud Khamis, akimkabidhi Katibu Mkuu wa
Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, cheti cha heshima kutokana na
uongozi wake.
Baadhi
ya viongozi na wanachama wa CUF waliojitokeza katika hafla ya
kumkabidhi fedha Maalim Seif iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni. (Picha
na mwandishi wetu)
Na: MWANDISHI WETU
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
amethibitisha nia yake ya kugombea tena nafasi ya Urais wa Zanzibar
katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza
katika hafla iliyoandaliwa na kamati maalum ya (CUF) Zoni ya Mjini
iliyokwenda kumdhamini kugombea nafasi hiyo huko nyumbani kwake Mbweni,
Maalim Seif amesema anatarajia kugombea tena nafasi hiyo ili aweze
kutimiza ndoto yake ya kuwatumikia wananchi.
