Shaban 1436
Leo ni Jumatatu tarehe 6 Shaban mwaka 1436 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 25 Mei 2015 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 52 iliyopita, hati ya Muungano wa Nchi Huru za Afrika OAU ilitiwa saini kwa kuhudhuriwa na nchi 30 za Kiafrika na kwa mantiki hiyo kukawa kumeandaliwa uwanja wa kuasisiwa taasisi ya kuziunganisha pamoja nchi za Kiafrika. Waasisi wa jumuiya hiyo walikuwa, Marais Jamal Abdul Nasser wa Misri, Kwame Nkrumah wa Ghana na Ahmed Sekou Toure wa Guinea. Jumuiya hiyo ilifanya juhudi za kuleta umoja baina ya nchi za Kiafrika, kuzikomboa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni na kutatua hitilafu pamoja na mifarakano baina ya nchi wanachahama. Mwaka 2002 viongozi wa OAU walikutana nchini Afrika Kusini na kubadilisha jina la taasisi hiyo muhimu barani Afrika na kuwa Umoja wa Afrika (AU). Hivi sasa umoja huo una wanachama 54 na makao makuu yake yapo mjini Addis Ababa Ethiopia. Siku hii ya tarehe 25 Mei inajulikana pia kwa jina la Siku ya Afrika.
Siku kama ya leo miaka 111 iliyopita muafaka na tarehe 6 Shaban mwaka 1325 Hijria aliuawa shahidi mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Khoei. Katika kipindi cha ujana wake alijibidiisha katika kutafuta elimu na aliweza kusoma kwa maulama wakubwa wa zama zake kama vile Sheikh Murtadha Ansari na kufikia daraja ya Ijtihad. Sheikh Ibrahim Khoei mbali na kutabahari katika masomo ya dini tukufu ya Kiislamu, alijikita zaidi katika elimu ya falsafa. Msomi huyo alikuwa mstari wa mbele kupinga dhuluma na uonevu na kutokana na harakati hizo, mfalme Mohammad Ali Shah wa silsila ya Waqajari alituma vibaraka wake na kumuua Shahidi allama Ibrahim Khoei
Na siku kama ya leo miaka 655 iliyopita yaani Mei 25 1360, kundi moja la mabaharia kutoka Ufaransa liliigundua Ghuba ya Guinea. Ghuba ya Guinea ipo magharibi mwa bara la Afrika katika bahari ya Atlantic. Muda mfupi baada ya kugunduliwa Ghuba hiyo, Wafaransa walianza upenyaji wao barani Afrika na taratibu wakaidhibiti ardhi iliyokuja kujulikana baadaye kwa jina la Guinea. Hatimaye mwaka 1958 Guinea ilijipatia uhuru wake baada ya harakati na mapambano ya wanaharakati na wapigania uhuru wa nchi hiyo kuzaa matunda

No comments:
Post a Comment