soundcloud

SAHAMA HAMAD 18 - Pata taarifa mbalimbali za Kisiasa, Uchumi, Dini pamoja na simulizi mbali mbali za kusikitisha zikiambatana na Makala pamoja na Tahrir za Kusisimua.. Pia tuwasiliane kupitia +255659887692 AHSANTENI...

Tuesday, 12 May 2015

Leo ni Jumanne tarehe 23 Rajab 1436 Hijiria inayosadifiana na tarehe 12 May 2015 Milaadia.

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/586a174104efc1b79b2cb91c21dbad1b_XL.jpg

Siku kama ya leo miaka 195 iliyopita, alizaliwa Florence Nightingale, mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa huko Florence nchini Italia. Nightingale aliyejulikana kwa jina mashuhuri la 'mwanamke mwenye taa mkononi' alikuwa muuguzi na mwanahesabati mashuhuri wa Uingereza. Alipewa lakabu ya 'mwanamke mwenye taa mkononi' kutokana na uvumilivu wake mkubwa na kujinyima usingizi kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa nyakati za usiku. Alifanya juhudi kubwa pia kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika hospitali nyingi za nchini Uingereza. Kazi hiyo aliyoifanya kwa miaka mingi bila kuchoka bila shaka ilimdhoofisha sana kimwili kwa kadiri kwamba alikuwa kipofu mwishoni mwa umri wake ambapo hatimaye aliaga dunia tarehe 13 Agosti 1910 Milaadia.
******************
Siku kama ya leo miaka 70 iliyopita, Berlin mji mkuu wa Ujerumani iligawanywa katika sehemu mbili za Mashariki na Magharibi. Kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa baada ya kumalizika Vita vya Pili vya Dunia kati ya serikali nne zilizoiteka Ujerumani, mji huo uligawanywa na kudhibitiwa na serikali hizo za Russia, Ufaransa, uingereza na Marekani. Muda mfupi baadaye mji huo ukadhibitiwa na Urusi ya zamani. Harry Truman rais wa wakati huo wa Marekani alichukua uamuzi wa kuvunja mzingiro na udhibiti huo wa Urusi. Katika kutekeleza hatua hiyo Marekani ilikaribia kupigana vita na Urusi. Matokeo mengine ya hali hiyo ilikuwa ni kugawanywa Ujerumani katika sehemu mbili za Ujerumani Magharibi na Mashariki.
*************
Siku kama ya leo Miaka 45 iliyopita na kwa mujibu wa azimio nambari 278 la Umoja wa Mataifa nchi ya Bahrain ilitengwa na ardhi ya Iran. Kabla ya kudhihiri Uislamu, nchi hiyo ndogo iliyo katika Ghuba ya Uajemi ilikuwa katika utawala wa Iran na baada ya kubuniwa utawala wa Kiislamu ikawa inadhibitiwa na makhalifa wa Kiislamu. Mwanzoni mwa karne ya 7 Hijiria kwa mara nyingine tena nchi hiyo iliunganishwa na Iran na baada ya hapo ikawa chini ya himaya ya Uingereza. Licha ya hayo Iran iliendelea kudai udhibiti na utawala wake kwa Bahrain na kulalamikia vikali hatua ya Uingereza ya kuitawala nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment