#WAJITOA.
Umoja wa ulaya ambao ni mfadhili mkuu wa serikali ya Burundi hii leo umetangaza kusimamisha misaada ya moja kwa moja kwa serikali ya nchi hiyo kufuatia kushindwa kutimiza matakwa ya Umoja huo kutokana na rekodi yake katika masuala ya haki za binadamu.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini alisema katika taarifa yake kuwa suala la hali ya kisiasa nchini Burundi linaendelea kuwa jambo la msingi kwa umoja huo na kuwa ili mahusiano kati yaserikali ya nchi hiyo na Umoja huo yarejee katika hali ya kawaida serikali ya Burundi itapaswa kuchukua hatua madhubuti za kurekebisha hali ya sasa.
Mongherini amesema serikali ya Burundi inapaswa kutekeleza hatua ilizokubaliana nazo na Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika mashariki na Umoja wa mataifa na kuzungumza na upinzani ili kutafuta suluhisho mwafaka la kisiasa kwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment