#CUF WASIKITISHA NA KINACHOENDELEA ZANZIBAR.
imetolewa leo Tarehe 16/03/2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
VIPIGO NA KAMATA KAMATA ZANZIBAR SIO TU NI UKIUKAJI WA HAKI ZA BINADAMU LAKINI PIA NI FEDHEHA KWA TANZANIA.
CUF Chama cha Wananchi kinasikitishwa na Hali tete inayowakabili Wakazi wa Visiwa vya Pemba na Unguja kutokana na Vipigo na Kamata Kamata inayoendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vikosi vya SMZ. Cuf haioni sababu ya vipigo hivyo kwa Raia Hao hasa ukizingatia Uwepo wa wa Asikari wengi kwenye Visiwa hivyo jambo ambalo linawapa uwezo wa kumkata Mualifu au mtuhumiwa uhalifu bila ya Kipigo na kumfikisha Mahamani.
CUF Chama cha Wananchi kinalaani vikali uvamizi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwenye Ofisi za Cuf zilizopo Mpandae, ambapo pamoja na kukamatwa Viongozi na Wanachama wetu Lakini pia uharibifu wa Mali na Vitendekazi kama Vile Computer umefanyika.
Vipigo vinavyoendelea katika Visiwa vya Pemba na Unguja, sio tu ni ukiukaji wa Haki za Binadamu Lakini pia ni Fedha kwa Taifa letu. Mambo haya yalifanywa na Serikali ya Makaburu dhidi ya Wazalendo wa Afrika Kusini kwa Misingi ya Ubaguzi wa Rangi. Ni aibu na Fedheha ya Hali ya juu, mambo kama hayo kufanywa na Serikali ya Kizalendo ya Tanzania dhidi ya Raia wake kwa kisingizio cha Kulinda Amani.
CUF Chama cha Wananchi hakipingi dhana ya kulinda, Lakini dhana hiyo ni vyema ika akisi Machoni na kwenye Masikio ya Watu. Huwezi kudumisha au kulinda Amani kwa Vipigo visivyo na sababu. Kupiga Walala Hoi, au kupiga Marofa na Makabwela kwa hoja yoyote ile sio tu kutarejesha Uhasama Visiwani humo Lakini pia kutaathiri Shughuli za Kimaendeleo na Ukuaji wa Demokrasia.
CUF Chama cha Wananchi, kinawakumbusha Marais Wastaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar, na hasa Mh Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, kukumbuka Muafaka baada ya Matukio ya January 26 na 27 Mwaka 2001. Tulisameheana lakini tukasisitiza tusiyasahu Matukio yale, Kwani Kusahau kunaweza pelekea kuyarejea.
Marais Wastaafu kwa kushirikiana na Rais aliopo Madarakani, mnaweza kuelekeza namna Bora na isio na athari katika kutekeleza dhana ya Kulinda Amani Visiwani Zanzibar. Kuhusu kile kinachoitwa Marejeo ya Uchaguzi,
CUF Chama cha Wananchi msimamo wetu upo pale pale, Majina ya waliokua Wagombea wetu kuendelea kuwepo kwenye Karatasi za kupiga Kura si hoja kwetu wala kwa Wapiga Kura wetu. Hoja yetu kwa Sasa ni Kuimarisha Chama Chetu ili kuendelea kudai Haki zetu.
Kuhusu Afya ya Maalim Seif ambae ni Katibu Mkuu wetu inazidi kuimarika kwa Kasi na Muda si mrefu Madaktari wake tunategemea watapojiridjisha kutokana na Muda waliomshauri kupumzika, watqmruhusu kuendelea na Shughuli zake.
HAKI SAWA KWA WOTE
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Habari/Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF Chama cha Wananchi
No comments:
Post a Comment